• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Ustawi wa Jamii
    • Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

"Fanyeni kazi kwa bidii mradi ukamilike kwa wakati"- RC Senyamule

Tarehe iliyowekwa: March 24th, 2023

Vijana wanaofanya kazi ya ujenzi wa majengo matatu katika Hospitali ya Mji Kondoa wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha mradi kwa wakati na kutoa huduma kusudiwa kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akikagua ujenzi wa majengo hayo pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa na wilayani wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kondoa hivi karibuni.

”Vijana mnajua kuna changamoto ya ajira Mhe. Rais akileta fedha hizi faida kubwa mojawapo ni vijana kupata ajira kama nyie mlivyopata sasa mmesikia mradi huu unamwisho hautakiwi kuchukua muda mrefu kuukamilisha na nyie mpo site,”amesema Mhe. Senyamule

Aidha amewataka kufanya kazi kwa muda mrefu ili watumie muda mfupi unaobakia kupumzika hali itakayowasaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuhifadhi fedha zitakazowasaidia pia kutunza familia zao ikiwa ni pamoja na kwenda kuwaambia wenzao mambo mazuri yanayofanywa na serikali na faida walizopata kuwepo katika mradi huo.

Aidha Mkuu wa mkoa ameagiza vifaa vyote kwa ajili ya ujenzi viwepo eneo la ujenzi na kuachana na mazoea ya kununua vifaa kidogo kidogo kama zamani kwakuwa Mhe. Rais ameleta fedha zote za mradi na kutaka kuukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.

Akiongea kwa niaba ya vijana wengine Ndg. Joel Laizer amesema mradi huo umewasaidia kupata ajira inayofasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kiafya kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo.

Akisoma awali taarifa ya ujenzi wa mradi huo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Emiliana Donald amemshukuru Mhe. Rais kwa kuapatia fedha hizo za ukarabati a Hospitali ambapo kutokana na majengo ya awali kuwa katika hali hiyo iliwalazimu kuomba kibali cha kujenga majengo matatu ili fedha inayobakia ifanye ukarabati kwa majengo mengine.

“Mhe. Mkuu wa mkoa tumeanza na kujenga majengo matatu ambayo ni jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto na mochwari kwa kuwa ya awali yalikuwa katika hali mbaya ambapo yakikamilika yatasaidia sana katika kuboresha hali ya utendaji kazi katika hospitali yetu,”amesema Dkt. Emiliana

Ziara ya Mkuu wa Mkoa imefanyika wilayani Kondoa ambapo katika Halmashauri ya Mji Kondoa ametembelea katika Zahanati ya Mtaa wa Ausia na ujenzi wa Hospitali ya Mji Kondoa ambapo aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa na wataalam wa mkoani.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya Katibu Muhtasi na Madereva Halmashauri ya Mji Kondoa February 24, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha nne Shule za Halmashauri ya Mji Kondoa January 29, 2023
  • Waliochaguliwa na shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2023 Kondoa Mji December 14, 2022
  • Tangazo la kazi December 07, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Wadau wa huduma ndogo za kifedha Kondoa Mji wapatiwa mafunzo

    May 26, 2023
  • Wanafunzi Chuo Kikuu cha Ardhi watembelea la akiba Mkungunero

    May 18, 2023
  • LIHOGOSA MICRO-CREDIT CO. LTD Kondoa wapewa siku tatu kuboresha huduma zao

    May 16, 2023
  • RAS Gugu ahimiza upendo na ushirikiano sehemu ya kazi

    May 03, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Fursa za uwekezaji Kondoa Mji
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa