• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkurugenzi awataka Wakuu wa Shule kuwajibika

Tarehe iliyowekwa: January 6th, 2021

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Msoleni Juma Dakawa amewataka wakuu wa shule kuwajibika katika majukumu waliyopewa ili kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika shule wanazoziongoza.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha kujadili mikakati ya kuinua elimu ya sekondari ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo la Uwekezaji hivi karibuni.

"Kila mmoja akawajibike kwenye eneo lake kwa kufanya kazi zilizopo katika barua yake ya uteuzi na ikiwezekana uwe unaweka tiki kila unalolitekeleza lakini hii haiukuzuii wewe kutofanya mengine ambayo unaona ni mazuri kwa ustawi wa shule yako," amesema Mkurugenzi Dakawa

Aidha amesikitishwa na tabia ya baadhi ya wakuu wa shule kutokuwa na mahusiano mazuri na walimu wao na kuwafanya wawaogope kuwafikia jambo ambalo linapelekea walimu kufanya kazi kwa manung'uniko na kutofurahia kazi.

"Mkuu wa Shule unapewa posho ya madaraka kila mwezi unashindwa kutoa hata shilingi elfu thelathini ukawanunulia kahawa, sukari na gesi walimu wako wakanywa chai ofisini? Lakini kwa ajili ya ubinafsi tunawaacha walimu wetu na njaa wataweza kufundisha wanafunzi wakafaulu vizuri?" ameuliza Mkurugenzi Dakawa

Hata hivyo amewataka Maafisa Elimu Kata kwenda katika shule zote na kukagua kwani walimu hawawajibiki kwa kuwa wao hawaendi kukagua na ndio hali iliyopelekea  wanafunzi kufeli japokuwa wengine wamepewa na usafiri.

"Tatizo tunafanya kazi  kwa mazoea ndio maana hatuwajibiki mjue yatatupeleka pabaya kwenye magroup yenu mnajadili vitu visivyo na tija katika kazi zenu mnajadili watu badala ya kujadili jinsi gani mtainua elimu katika shule zenu mbadilike mwaka huu si wa mchezo tena tumechoka Dodoma kuwa wa mwisho kila mwaka,"amesisitiza Mkurugenzi Dakawa

Ameongeza kwa kuwaagiza wote kuhakikisha wanafunzi wanaanza masomo mara tu shule zitakapofunguliwa na kuhakikisha wote wanafunzi wanakaa katika madawati kuanzia wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ikiwa ni pamoja na kuacha kupiga dili katika miradi inayopelekwa na serikali.

"Nendeni mkagawe majukumu kwa wasaidizi wenu wanaweza wale na wakifanya vizuri sifa zinakuja kwako, waheshimuni na muwatie moyo kwa kazi kubwa wanayofanya msifanye kazi kama vita mshirikiane nao wakati wa shida na raha bila kufanya hivyo ni ngumu sana wao kufundisha,"amesema Mkurugenzi Dakawa

Akitoa shukrani Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Kondoa Mwalimu Annete Nara amemshukuru Mkurugenzi kwa kuwafungulia kikao na kutoa mikakati mizuri yenye lengo la kuinua ufaulu kwa kuwa wameaminiwa.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Kondoa Islamic Mwalimu Salum Mwariko amemuahidi Mkurugenzi kuendelea kushirikiana na walimu wengine ili kuinua ufaulu kutokana na malengo waliyojiwekea na kusema kuwa watafanya marekebisho katika njia ya kufikia malengo inawezekana kuna sehemu walikwama lengo ili kufikia ufaulu unaostahili.

" Pia nachukua fursa hii kumshukuru Mkurugenzi kwa kutusaidia ujenzi wa barabara kuelekea shuleni tulifuatilia kwa kipindi kirefu TARURA lakini hawakulifanyia kazi hadi tulipomuona na akalifanyia kazi siku hiyohiyo na leo barabara imeanza kutengenezwa kiukweli kunamshukuru sana,"amesema Mwalimu Salum

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa