• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mwenge Wawakumbusha Wazazi Wajibu Wao kwa Wanafunzi

Tarehe iliyowekwa: August 3rd, 2018

Wazazi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa kuwapatia mahitaji ya shule watoto wao ili waweze kusoma vizuri na kupata elimu iliyo bora.

Hayo yalizungumzwa na mkimbiza Mwenge kitaifa Bwana Charles Kabeho wakati akitoa ujumbe wa mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Mji wa Kondoa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Msui.

“Wazazi hamuwezi kukwepa jukumu la kuwanunulia sare wanafunzi hasa wa Shule za Msingi ambao wengi utawaona wamevaa sare zimetoboka na mashati hayana vifungo tofauti na wanafunzi wa sekondari au kwa kuwa wao wanajitambua wanadai sare pindi zinapochoka?”Aliuliza Kabeho

Aliongeza kuwa kama Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 unasisitiza masuala ya elimu hivyo wazazi pia wana jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili kuwaongezea nguvu ambayo itapelekea kuongeza uelewa wanapofundishwa ambapo kwa sasa ni Mikoa ya Njombe na Kilimanjaro tu ndiyo inawapatia chakula shuleni wanafunzi kwa zaidi ya asilimia tisini.

Aidha aliwasihi wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kuwafuatilia mahudhurio yao shuleni na madaftari yao ili kujua iwapo mtoto ana tatizo na baadhi ya masomo na hatimaye aweze kuwasiliana na mwalimu wa somo husika na kumuelewesha ili  apate elimu bora na yenye manufaa kwa mtoto.

Hata hivyo aliwasisitiza wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao waliohitimu kwenye vyuo vya ufundi ikiwemo VETA na vyuo ya Maendeleo ya Jamii ili wapate ujuzi ambao utasaidia wao kujiajiri au kuajiriwa na kuendana na dhana ya nchi ya  viwanda na kuboresha uchumi kwa kufikia uchumi wa kati.

“Shule hii ina wanafunzi wachache sana ukilinganisha na shule zingine jambo ambalo halikubaliki wazazi hata kama wengi ni wafugaji hapa lakini wapelekeni watoto shuleni ni haki yao na ifikapo Januari 2019 hakikisheni watoto wote wanaenda shule ili wapate elimu ambayo ni ufunguo wa maisha yao na serikali imeendelea kuwekeza huko kwa kujenga madarasa, nyumba za walimu na maabara.”Alisisitiza Kabeho alipoongea na wazazi wa Kijiji cha Munguri.

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Halmashauri ya Mji Kondoa siku ya tarehe 2 Agosti ukitokea Wilayani Chamwino ambapo umepitia miradi saba kwa kuzindua, kuona na kuweka jiwe la Msingi miradi ambayo ni Afya, Elimu, Maji, Uvuvi na Vikundi ikiwa imewezeshwa kwa fedha za serikali na mashirika ya dini na wawekezaji binafsi.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa