• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wananchi Kondoa Mji watolewa hofu hati yenye mashaka

Tarehe iliyowekwa: May 20th, 2021

Na: Leah Joseph

Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa Andrew Ng'wani amewatoa hofu wananchi wa Halmashauri ya Mji kondoa kutokana na kupata hati yenye mashaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hivi karibuni.

"Wengi tumepokea kwa masikitiko taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kuwa Kondoa ni miongoni mwa Halmashauri zenye hati yenye mashaka, niwatoe hofu kwamba hakuna kitu kilichoharibika na wala hakuna ubadhilifu wowote wa fedha za serikali uliofanywa na kiongozi yeyote ila ni changamoto ya takwimu ilijitokeza wakati wa uwasilishaji, "amesema Katibu Tawala.

Aliendelea kusema kuwa ana uhakika mwaka huu 2020/2021 Halmashauri ya Mji Kondoa itapata hati safi na kuondokana na sintofahamu inayojitokeza kwa watumishi pamoja na wananchi wote.

"Kama mlivyoona kuna mapendekezo 13 tumejadili yaliyo ndani ya uwezo wetu tutayafanyia kazi na ambayo yapo nje ya uwezo wetu  yatawasilishwa mahala panapohusika ili yaweze kupatiwa ufumbuzi,"amesisitiza Katibu Tawala Ng'wani.

Hata hivyo Katibu Tawala amewaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa mwaka huu kuna mbio za mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kukimbizwa wilayani Kondoa mwezi Julai mwaka huu.

"Niwaombe wajumbe wote pamoja na wadau kujitokeza kwa wingi katika kuupokea Mwenge wa Uhuru kwetu ni heshima kubwa sana kuna maandalizi mbalimbali yatafanyika hivyo kila mtu ajitokeze kutoa ushirikiano pale atakapohitajika kufanya hiyo, "amesisitiza Katibu Tawala Ng'wani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Kondoa Bw. Hussein Kova amewataka watumishi na viongozi  wote kufanya kazi kwa umoja na kuziacha tofauti zao kwani hakuna binadamu aliyekamilika.

"Tuache kufanya kazi kwa majungu na kusengenyana kwani kufanya hivyo ni kuikwamisha Wilaya na Halmashauri katika maendeleo mimi kama mwenyekiti sipo tayari kuona haya yanatokea, "amesisitiza Bw. Hussein Kova.

Ameongeza kuwa kama mtumishi au kiongozi yeyote amekosea ananmahala pake pa kusemewa na sio kwenye magenge kwani kila kitu kinaongozwa na sheria kanuni na taratibu zake lakini pia ameonya kuachana na makundi  katika maeneo ya kazi na kwamba badala yake watu wafanye kazi kwa juhudi na kushirikiana.

Kikao maalumu cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani kimefanyika ili kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa Mh. Mohamed Kiberenge na kuhudhuriwa na Katibu Tawala, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali toka makao makuu,Kaimu Mkurugenzi, Waheshimiwa Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama,  Wakuu wa Idara na Vitengo, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi pamoja na waandishi wa habari.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa