• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Kondoa Town Council
Kondoa Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Kondoa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Idara ya Mipango ,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu sekondari
      • Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
      • Idara ya Usafi na Mazingira
      • Divisheni
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Miundombinu Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Viwanda Bishara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Usimamizi na Utawala wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugi na Uvuvi
    • Kitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Teknolojia,Habari,Mawasiliano na uhusiano
      • Kitengo cha Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
  • Kituo cha habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wasira aelezea faida za Muungano kwa wananchi wa Kondoa

Tarehe iliyowekwa: April 26th, 2025

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Stephen Wasira ameeleza faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Suruke iliyopo Kata ya Suruke katika Halmashauri ya Mji Kondoa.

Wasira ameeleza kuwa Muungano unachochea na kuimarisha biashara baina ya pande mbili lakini pia unaleta aman kwani wananchi wa pande zote mbili wanauhuru wa Kwenda kuishi katika nchi hizo mbili bila masharti yoyote.

Aidha amewapongeza viongozi waasisi wa Muungano huo ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Hayati Abeid Amani Karume kwa kuona mbali na kuziunganizha nchi hizi mbili ambapo matunda yake yanaonekana hadi leo.

Hata hivyo amewasihi wananchi kuendelea kuudumisha na kuuenzi Muungano huo ili kuendeleza maono ya viongozi waasisi na kudumisha amani na kukemea wote wanaobeza Muungano kwani hawana nia njema na maendeleo ya wananchi na nchi hizo mbili.

Hata hivyo Wasira ameongeza amewakumbusha wananchi wote ambao bado hawajajiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura kutumia fursa ya kujiandikisha itakapokuja awamu ya pili mapema mwezi Mei Ili kila mmoja apate haki yake ya kikatiba ya kuchagua kiongozi amtakaye katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kondoa Ndg. Said Majaliwa akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo kwa Makamu Mwenyekiti ametumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhatI kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya milioni 544 kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Suruke.

“Ujenzi wa Shule ya Sekondari Suruke umelenga kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu lakini pia kutoa wigo mpana wa kila mtu kupata elimu Ili kuwa na kizazi kilichoelimika zaidi”amesema Mkurugenzi Majaliwa

Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM bara imefanyika wilayani Kondoa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo hufanyika kila tarehe 26 Aprili ya kila mwaka ambapo mwaka huu ni miaka 61 toka kutokea kwake na  kauli mbiu ya mwaka huu imesema “Muungano wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa Shiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Matangazo

  • Tangazo la mikopo inayotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu February 21, 2025
  • Matokeo ya kidato cha nne 2024 shule za Sekondari Kondoa Mji January 23, 2025
  • Tangazo la kushiriki mazoezi ya kila Jumamosi ya pili kila mwezi January 02, 2025
  • Tangazo la umilikishwaji viwanja January 02, 2025
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la awali ngazi ya kata yatolewa kwa Watendaji Kondoa Mji

    May 14, 2025
  • RC, RAS, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Dodoma ziarani Mufindi kujifunza kilimo cha Tufaa (Apple)

    May 11, 2025
  • Mkurugenzi Majaliwa aagiza miradi kukamilika ifikapo Mei 31

    May 08, 2025
  • ALAT mkoa wa Dodoma yatembelea miradi ya maendeleo Kondoa Mji

    May 03, 2025
  • Tazama Vyote

Video

Matukio ya Mwenge wa Uhuru Kondoa Mji 2025
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Mpango Mkakati
  • Maktaba ya Picha
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Sheria ndogo
  • Ripoti Mbalimbali
  • Fomu Mbalimbali
  • Miradi Inayoendelea

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea Tovuti

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Kwapakacha

    Anuani ya Posta: S.L.P 711

    Simu ya Mezani: +255 712264912

    Simu ya Mkononi: +255 712264912

    Barua Pepe: td@kondoatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Kondoa - Haki Zote Zimehifadhiwa